Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WATUMISHI WALIOHAMA NA KUSTAAFU WAAGWA
WATUMISHI WALIOHAMA NA KUSTAAFU WAAGWA Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah J. Mugeta ameongoza Watumishi wa Shirika Makao Makuu na wale wa Kanda ya Dodoma katika hafla fupi ya Kumuaga Mtumishi aliyestaafu Ndg Fabiani Kisse Pamoja na Bi. Perpetua Shumbu ambaye anahamia katika ofisi za Wizara ya Kilimo, Hafla hiyo imefanyika tarehe 01 Julai 2025 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika uliopo Jijini Dodoma CPA Mugeta amesema “Tunawashukuru sana kwa mchango wenu mkubwa katika maendeleo ya Taasisi hii. Mlifanya kazi kwa bidii na kujituma, na tumejifunza mengi kutoka kwenu. Tunawaombea kila la heri katika safari zenu mpya na maisha yenu mapya.”