MWALIKO WA MAFUNZO YA SIKU TATU KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA KUHUSU UHASIBU, UKAGUZI WA NDANI NA MATUMIZI YA ‘AI’ (21–23 JANUARI 2026)
http://www.coasco.go.tzMWALIKO WA MAFUNZO YA SIKU TATU (21–23 JANUARI 2026)
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO). linawaalika viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo ya siku tatu yatakayofanyika kuanzia tarehe 21 hadi 23 Januari 2026.
Mafunzo haya yatahusu uhasibu, ukaguzi wa ndani, pamoja na matumizi ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) katika kuboresha usimamizi wa fedha na mifumo ya taarifa ndani ya Vyama vya Ushirika. Mafunzo yamelenga kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika uendeshaji wa Vyama vya Ushirika.
Ada ya Ushiriki:
Kila mshiriki anatakiwa kuchangia ada ya Tshs 350,000, ambayo inajumuisha gharama za mafunzo ya siku tatu, ukumbi, chai na chakula cha mchana wakati wa mafunzo.
Malipo yatalipwa kupitia nambari ya malipo ya Serikali itakayotolewa baada ya kuthibitisha ushiriki wako kwa kuwasiliana na RCA au Mratibu wa Mafunzo (CPA Gabriel Msuya) kupitia simu 0762 389 616 au barua pepe gabriel.msuya@coasco.go.tz.
Imetolewa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO).
