Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
KIKAO CHA 84 CHA BODI YA WAKURUGENZI - COASCO
KIKAO CHA 84 CHA BODI YA WAKURUGENZI – COASCO Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limefanya Kikao cha 84 cha Bodi ya Wakurugenzi tarehe 25 Novemba 2025, katika Ukumbi wa PSSSF, Dodoma. Kikao hicho kimelenga kupitia utekelezaji wa majukumu ya shirika, kufanya tathmini ya maendeleo ya kimkakati, pamoja na kujadili masuala muhimu ya kiutawala na kiutendaji. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, CPA Juma A. Kimori, ambaye ameongoza mijadala muhimu kuhusu mwelekeo wa shirika, uboreshaji wa huduma kwa vyama vya ushirika, na utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka wa fedha. Bodi imepongeza hatua zinazochukuliwa na Menejimenti katika kuboresha huduma na kuimarisha uhusiano na wadau wa sekta ya ushirika, sambamba na kuendelea kuweka msingi imara wa ustawi wa shirika. COASCO inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama chombo muhimu katika kuimarisha uwazi, uadilifu na maendeleo ya vyama vya ushirika nchini.