Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
Historia ya Coasco

Uanzishwaji wa Shirika

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa Sheria Na.15 ya mwaka 1982 kwa lengo la kutoa huduma  za Ukaguzi na Usimamizi kwa Vyama vya Ushirika  Tanzania.

Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2005 ili kupanua wigo wa huduma za Shirika za Ukaguzi na Ushauri kutolewa kwa Vyama vya Ushirika pamoja na Taasisi za Umma,   Makampuni binafsi, Mabenki na wateja wengine wasio Ushirika.

Shirika linatambulika na Bodi ya Wakaguzi na Wahasibu Tanzania (NBAA) kama ni Shirika la kitaaluma na kupewa hati ya kutoa huduma za ukaguzi na ushauri kwa kufuata misingi ya taaluma ya ukaguzi na uhasibu.