Majukumu yetu
Malengo yaliyoidhinishwa ya Shirika kama ilivyoainishwa chini ya Sehemu ya 4 ya Sheria yake wezeshi, inaipa COASCO mamlaka kisheria kutoa huduma zifuatazo kwa wateja mbalimbali:
i. Ukaguzi wa taarifa za fedha kwa wateja mbalimbali
ii. Kufanya uchunguzi kwa wateja
iii. Kutoa huduma za ushauri wa kodi na usimamizi kwa wateja
iv. Kuendesha mafunzo ya kazi/vitendo kwa vyama vya ushirika kuhusu utunzaji wa vitabu vya hesabu na utayarishaji wa taarifa za fedha kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Kuripoti Taarifa za Fedha (IFRSs)
v. Kutoa huduma ya kazi ya uhasibu kwa wateja ikiwa ni pamoja na kubadilisha taarifa za fedha kuwa IFRs
vi. Mafunzo juu ya IPSAs na IFRSs
vii. Mafunzo juu ya ISA na mafunzo ya kazi juu ya ukaguzi wa ushirika
viii. Kuendesha mafunzo ya kazi kwa wateja juu ya ukaguzi wa ndani
ix. Kufanya utafiti wa utendaji wa vyama vya ushirika na kuishauri serikali ipasavyo