-
JENGO LA OFISI YA COASCO MAKAO MAKUU
Muonekano wa Jengo la ofisi za Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) lilipo mjini Dodoma ambapo ndio Makao makuu
-
MKUTANO WA WAKAGUZI WA USHIRIKA WA MIKOA
Picha ya pamoja baada ya Mkutano wa Wakaguzi wa Ushirika wa Mikoa (RCA's) na Menejimenti ya COASCO iliofanyika Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma siku ya alhamisi na ijumaa kuanzia tarehe 18 hadi 19 mwaka 2022
-
MKUTANO WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI
Menejimenti ya COASCO pamoja na Wajumbe wa Baraza kuu la wafanyakazi COASCO wakiwa kwenye picha ya pamoja baada Mkutano kilichofanyika Tarehe 28/10/2022 Ukumbi wa Maktaba jijini Dodoma
-
KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO Ndugu Yona Killagane akiwa kwenye kikao na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejementi ya COASCO Kilichofanyika tarehe 16.12.2022 katika ukumbi wa LAPF Mjini Dodoma
-
Bodi ya usimamizi wa vyama vya ushirika yajengewa uwezo
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika(COASCO), CPA Yona Kilagane, ameushukuru uongozi wa Taasisi ya Uongozi kwa kutoa mafunzo ya Usimamizi bora wa Mashirika ya Umma yatakayowajenga uwezo watendaji katika usimamizi wa Vyama vya Ushirika.
-
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO wakiwa katika Semina juu ya Majukumu ya Bodi katika Taasisi za Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Uongozi jijini Arusha tarehe 17 hadi 19'Januari 2023
-
KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI COASCO KUJADILI BAJETI YA SHIRIKA MWAKA 2023/2024
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO, CPA Ndugu Yona Killagane waliokaa upande wa kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejementi ya COASCO baada ya kikao cha bajeti Kilichofanyika tarehe 27.04.2023 katika ukumbi wa LAPF Mjini Dodoma
-
WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO wakiwa kwenye kikao cha kujadili Bajeti ya Shirika ya mwaka wa Fedha 2023/2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma tarehe 27.04.2023
-
WATUMISHI WA COASCO WAKITOA ELIMU SIKU YA USHIRIKA DUNIANI
Watumishi COASSCO wakitoa elimu kwa wateja waliotembelea katika banda la Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani SUD, ipuli Tabora 2023
-
WATUMISHI WA COASCO WAKITOA ELIMU KWA WADAU WA USHIRIKA SUD TABORA
Watumishi wakimsikiliza mmoja wa wadau waliokuwepo kwenye maadhimisho ya SUD 2023
-
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO CPA J.J. MUGETA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAZIRI WA KILIMO.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO CPA J.J. Mugeta akitoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa Shirika kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alipotembelea katika banda la Shirika wakati wa Maadhimisho ya sherehe ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) 2023, Ipuli Tabora.
-
WAZIRI WA KILIMO AKITOA MAELEKEZO KWA KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA COASCO.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa COASCO CPA J.J. Mugeta kuwa “Bodi ya TCDC na Bodi ya COASCO wakae pamoja ili kuweza kuandaa mikakati ya kupunguza changamoto zinazotokea katika vyama vya Ushirika.”
Mhe. Bashe aliyasema hayo wakati wa maonesho ya
-
WAZIRI WA KILIMO ALIPOTEMBELEA KIJIJI CHA USHIRIKA KWENYE MAONESHO YA NANENANE 2023 MBEYA.
Waziri wa Kilimo Mhe, Hussein Bashe akisaini kwenye kitabu cha Wageni wakati wa Ziara yake katika mabanda ya Kijiji cha Ushirika kwenye Maonesho ya Nanenane 2023 Jijini Mbeya.
-
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AKIONGEA NA MRAJIS NA MTENDAJI MKUU WA TCDC.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO CPA J.J. Mugeta akitoa maelezo mbalimbali yanayohusu Shirika hilo kwa Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dr. Benson Ndiege, alipotembelea banda la Shirika kwenye Maonesho ya Nanenane 2023 Jijini Mbeya.
-
KAIMU MKURUGENZI WA UKAGUZI CPA GOLDEN KAJABA AKIONGEA NA MDAU.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi CPA Golden Kajaba akitoa ufafanuzi kuhusu Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika wa mwaka 2022/2023 kwa mmoja wadau waliotembelea banda la COASCO kwenye Maonesho ya Nanenane 2023 Jijini Mbeya.
-
MWENYEKITI WA TFC ALIPOTEMBELEA BANDA LA COASCO NANENANE 2023 MBEYA
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vya Ushirika Tanzania (TFC), Charles Jishuli, akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika CPA J.J. Mugeta wakati wa Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
-
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO 2023, MWANZA
KAIMU MKURUGENZI WA COASCO CPA J.J MUGETA AKITOA UFAFANUZI WA AINA ZA HATI KWA MRAJIS NA MTENDAJI MKUU WA TCDC DR. BENSON NDIEGE KWENYE MAADHIMISHO YA KIMATAIFA YA SIKU YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO 2023, YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA FURAHISHA JIJINI MWANZA
-
ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA KWENYE MAADHISHO YA ICUD 2023
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg Balandya Elikana, ameipongeza COASCO kwa kazi nzuri ya ukaguzi, usimamizi na ushauri wanaoutoa kwa vyama vya Ushirika, alipotembelea banda la Shirika katika maadhimisho ya siku ya ushirika wa akiba na mikopo Duniani (ICUD) katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza
-
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AHUDHURIA KIKAO KAZI CHA WIZARA
Kaimu Mkurugenzi wa COASCO, CPA J.J Mugeta alihudhuria katika kikao kazi na Waziri wa Kilimo Mhe, Hussein Bashe (Mb) kilichojumuisha Wenyeviti na Watendaji wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika leo Oktoba 31 Jijini Dodoma.
-
MAFUNZO KWA WATENDAJI WA SACCOS MOROGORO
Shirika la COASCO limetoa mafunzo kwa Watendaji wa Saccos yenye lengo la kuwajengea uwezo na ujuzi katika masuala ya Uhasibu na Ukaguzi yanayofanyika kuanzia tarehe 21 - 23 Novemba 2023, Mjini Morogoro