Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UBIA (PPP)
12 Mar, 2026
MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UBIA (PPP)

MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UBIA (PPP)

Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imepatiwa mafunzo kuhusu uwekezaji wa miradi ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) kwa lengo la kuongeza uelewa na ufanisi wa usimamizi wa miradi ya Shirika.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, leo Machi 11, 2026 katika ukumbi  wa Shirika Ofisi ya Dodoma Makao Makuu , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, CPA Jeremiah Mugeta, ameshukuru na kumpongeza Mkufunzi wa mafunzo hayo kwa uwasilishaji mzuri.

CPA Mugeta, amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kuelewa na kusimamia vyema utekelezaji wa mpango wa miradi ya ubia ya COASCO katika maeneo ya Upanga na  Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Makole jijini Dodoma pamoja na Songea.

Kwa upande wake, Mkufunzi wa mafunzo hayo, Edwin Kidiffu, amesema Serikali imekuwa ikitumia mfumo huo kama njia ya kuongeza ufanisi, ubunifu pamoja na kuboresha ubora wa huduma za umma.