KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AKABIDHIWA GARI JIPYA LA OFISI LITAKALOTUMIKA MAKAO MAKUU
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AKABIDHIWA GARI JIPYA LA OFISI LITAKALOTUMIKA MAKAO MAKUU
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Jeremiah Mugeta, amekabidhiwa gari jipya la ofisi aina ya Toyota Land Cruiser Hard Top (2026) lenye thamani ya Shilingi 235,667,552.67.
Gari hilo limenunuliwa na COASCO kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wadau.
Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 16, 2026 Makao Makuu ya COASCO, Dodoma ambapo Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, CPA Prisilla Mushi, alimkabidhi funguo pamoja na nyaraka za gari hilo.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, CPA Jeremiah Mugeta amesema ununuzi wa gari hilo ni sehemu ya mkakati wa COASCO wa kuendelea kuimarisha utendaji na kuboresha mazingira ya kazi.
Amesema kuwa gari hilo litatumika katika shughuli za Makao Makuu ya Shirika, na kusisitiza litunzwe na kutumika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Serikali ili liendelee kutoa huduma kwa manufaa ya shirika na wadau wake.
