Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WIZARA YA KILIMO, COASCO ZAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA UTENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA
09 Sep, 2026
WIZARA YA KILIMO, COASCO ZAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA UTENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Mhandisi Athumani Kilundumya; na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. M. Msoffe wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Alphonce Muro kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni ili kujadili mipango na mikakati ya Shirika hilo katika shughuli za kukagua na kuimarisha utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika nchini. Kikao hicho kimefanyika tarehe 8 Septemba 2026, katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.