Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
CPA JEREMIAH MUGETA ATUNUKIWA TUZO KWA UONGOZI WA MAONO NA MCHANGO WA KIPEKEE KATIKA MAENDELEO YA SHIRIKA
19 Jul, 2026
CPA JEREMIAH MUGETA ATUNUKIWA TUZO KWA UONGOZI WA MAONO NA MCHANGO WA KIPEKEE KATIKA MAENDELEO YA SHIRIKA

CPA JEREMIAH MUGETA ATUNUKIWA TUZO KWA UONGOZI WA MAONO NA MCHANGO WA KIPEKEE KATIKA MAENDELEO YA SHIRIKA

Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imemtunuku tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika, CPA Jeremiah Mugeta, kwa kutambua uongozi wake wenye maono na mchango wake wa kipekee katika kuchochea ukuaji, mabadiliko na ubora wa utendaji wa Shirika.

Tuzo hiyo imetolewa Julai 11, 2026 katika hitimisho la Kikao Kazi cha Menejimenti, Wakaguzi wa Mikoa na Wakaguzi wa Ofisi ya Makao Makuu kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Palace jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kaimu Meneja wa Ukaguzi, Peter Mushi, amesema tuzo hiyo ni kutambua mchango wa CPA Mugeta katika kuongoza mabadiliko chanya, kuimarisha mifumo ya utendaji na kusimamia jitihada za kuboresha utoaji wa huduma za ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika nchini.

Aidha, CPA Mugeta ameshukuru kwa kutunukiwa tuzo hiyo na kuasa watumishi wa Shirika kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili shirika lizidi kutoa huduma bora za ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya ushirika na Taasisi nyingine.