Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WANAWAKE WA COASCO WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
09 Mar, 2026
WANAWAKE WA COASCO WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WANAWAKE WA COASCO WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Watumishi wanawake wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wameungana na wanawake wenzao duniani kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika Mkoa wa Dodoma, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mbande, Wilaya ya Kongwa, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary S. Senyamule, alikuwa mgeni rasmi. 

Katika maadhimisho hayo, Mhe. Senyamule amesisitiza umuhimu wa jamii kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa katika elimu, ajira na maendeleo ya kiuchumi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Haki Sawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi wa Maendeleo Jumuishi Kufikia Dira 2050