Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WANAWAKE COASCO WAFARIJI WAKINA MAMA WALIOLAZWA DODOMA RRH
09 Mar, 2026
WANAWAKE COASCO WAFARIJI WAKINA MAMA WALIOLAZWA DODOMA RRH

WANAWAKE COASCO WAFARIJI WAKINA MAMA WALIOLAZWA DODOMA RRH

Wanawake wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wametembela na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kina mama wenye watoto wachanga na wanaookaribia kujifungua wanaopata matibabu kwenye wodi za wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (Dodoma RRH).

Msaada huo umejumuisha mahitaji mbalimbali ya kila siku yatakayowasaidia wakiwa wodini

Msaada huo umetolewa leo, Machi 7, 2026, ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma kwa wenye uhitaji wakati wakijiandaa na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.