Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAIPONGEZA MENEJIMENTI KWA KUBUNI MIRADI YA UWEKEZAJI WA UBIA
03 Mar, 2026
BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAIPONGEZA MENEJIMENTI KWA KUBUNI MIRADI YA UWEKEZAJI WA UBIA

BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAIPONGEZA MENEJIMENTI KWA KUBUNI MIRADI YA UWEKEZAJI WA UBIA

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imeipongeza Menejimenti ya Shirika hilo kwa kuwa na mpango wa kuanzisha miradi ya uwekezaji wa ubia (PPP) yenye lengo la kuongeza mapato ya ndani.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 27 Februari, 2026 katika Kikao cha 85 cha Bodi kilichofanyika katika Ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma, ambapo Mwenyekiti wa Bodi, CPA Juma A. Kimori, alipongeza kwa kubuni mpango huo wa uwekezaji utaoongeza mapato ya ndani ya Shirika.

Akizungumza katika kikao hicho, CPA Kimori amesema Bodi imeridhia mpango wa uwekezaji wa ubia katika maeneo ya Upanga Dar es Salaam, Chang’ombe, Makole Dodoma na Songea, ambapo kunatarajiwa kujengwa majengo ya ofisi za kupangisha, vyumba vya makazi (apartments) pamoja na maduka. Bodi imeridhia Menejimenti kuendelea na hatua zinazofuata kwa kuzingatia kikamilifu taratibu za Manunuzi ya Umma.

Pia Bodi imepitisha maboresho ya sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Shirika na Rasimu ya Kanuni za Utumishi, ili kuimarisha mfumo wa utawala bora na kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa Shirika.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, ameishukuru Bodi kwa pongezi hizo, akiahidi kuwa Menejimenti itatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Bodi.