Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
MENEJIMENTI YA COASCO YAWAJENGEA UWEZO VIONGOZI NA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA
22 Jan, 2026
MENEJIMENTI YA COASCO YAWAJENGEA UWEZO VIONGOZI NA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA

Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imewajengea uwezo viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kwa kutoa mafunzo maalum ya uhasibu, ukaguzi wa ndani pamoja na matumizi ya Akili Bandia (Artificial Intelligence - AI).

Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 23 Januari 2026 katika Ukumbi wa St. Gasper, Kisasa – Dodoma, yakihusisha washiriki kutoka vyama mbalimbali vya ushirika nchini.

Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa COASCO, CPA Prisilla Mushi, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, ambapo alisisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kuendelea kujengeana uwezo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mazingira ya kazi ya sasa.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuelimisha umuhimu wa kujengeana uwezo kwa viongozi na watendaji ili kuhakikisha maendeleo endelevu, uwazi, uwajibikaji, pamoja na matumizi sahihi ya teknolojia za kisasa katika uandaaji na usimamizi wa taarifa za fedha.

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamewezeshwa kupata maarifa ya vitendo yatakayosaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kila siku, hususan katika kusimamia rasilimali za wanachama kwa misingi ya kitaalamu na kidijitali