Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO MPYA WA e-Board
28 Jan, 2026
MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO MPYA WA e-Board

MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO MPYA WA e-Board


Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imepatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya wa e-Board, unaolenga kuboresha uratibu na uendeshaji wa vikao kwa njia ya mtandao


Mafunzo hayo yametolewa, Januari 27, 2026, katika Ofisi ya Makao Makuu ya Shirika yaliyopo Jijini Dodoma, na Mkufunzi kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Bi. Mwanamvua Rasi, ambapo amesema mfumo wa huo utaiwezesha Menejimenti kufanya vikao popote walipo bila ya ulazima wa kukutana ana kwa ana

“Mfumo wa e-Board utasaidia Menejimenti ya COASCO kuratibu na kufanya vikao mbalimbali kwa njia ya mtandao, hali itakayopunguza  gharama za uendeshaji wa vikao kutokana na kupungua kwa matumizi ya makaratasi,” amesema Mwanamvua

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah J. Mugeta, ameishukuru e-GA na pia kumpongeza mkufunzi huyo kwa kutoa mafunzo hayo, akisema kuwa yatasaidia kuongeza uwazi, ushiriki na ufanisi wa wajumbe katika vikao vijavyo