Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
ZIARA YA KIKAZI KUTOKA IDARA YA USHIRIKA ZANZIBAR
VIONGOZI WA USHIRIKA ZANZIBAR WAFANYA ZIARA COASCO DODOMA Viongozi na Watumishi wa Idara ya Ushirika Zanzibar wamefanya ziara ya mafunzo katika Ofisi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) Jijini Dodoma wakiwa na lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Ukaguzi pamoja na Elimu ya Uhasibu kwa Vyama vya Ushirika Ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 12 Machi 2025, ikiwahusisha Wanaushirika kutoka Zanzibar walioambatana na Viongozi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu katibu Mkuu, Kazi na Uwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Bi Halima Maulid Salum, amesema kuwa ziara hiyo imekuwa yenye tija na manufaa kwa pande zote mbili, kwani imewapa fursa ya kubadilishana mawazo na kujifunza jinsi ushirika unavyofanya kazi hususani katika kaguzi zake kupitia mfumo wa Ukaguzi wa hesabu wa COADMIS, na imewapa maarifa mapya ambayo yatasaidia kuboresha Vyama vya Ushirika Zanzibar na amewaalika Viongozi na wataalamu wa COASCO kutembelea Zanzibar kwa ajili ya kujifunza pia, Naye Kaimu Mkurugenzi wa COASCO CPA Jeremiah J. Mugeta amesema kuwa "Tunawashukuru kwa ziara yenu ambayo inatoa fursa ya Ushirikiano baina yetu na imefanyika katika wakati muafaka kwani kwa sasa COASCO tumeanza kutumia mfumo wa Ukaguzi wa kidigitali kwa kaguzi zetu zote kupitia mfumo wa COADMIS kwani mfumo huo unatuwezesha kurahisisha kazi zetu na hivyo kuongeza tija na ufanisi zaidi tena kwa wakati ikitofautishwa na mfumo tuliokuwa tukiutumia hapo awali"