Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AFUNGA MAFUNZO YA WADAU WA USHIRIKA
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO AFUNGA MAFUNZO YA WADAU WA USHIRIKA Mafunzo kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika yanayohusu masuala ya kodi na ukaguzi yaliyokuwa yanafanyika katika ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo hapa Jijini Dodoma yamefungwa rasmi tarehe 16 Mei, 2025 Akifunga mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) CPA Jeremiah J. Mugeta alisema “Mafunzo haya yamewaleta pamoja viongozi wa Bodi na Watendaji kutoka katika vyama mbalimbali vya Ushirika vikiwemo Saccos, Amcos, Vyama vikuu, Vyama vya miradi ya Pamoja na vyama vingine kwa lengo la kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ya usimamizi na uendeshaji wa vyama vya Ushirika hususani masuala ya kodi ya mapato Pamoja na ukaguzi kwa ujumla” Pia CPA Mugeta alisisitiza kuwa “Mafunzo hayo yalilenga kuwapa elimu kuhusu masuala muhimu yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kuandaa taarifa za fedha wakati wa ukaguzi hesabu zenu, jinsi ya kujibu hoja za ukaguzi na baada ya ukaguzi kufanyika ili kuondoa au kupunguza hoja za ukaguzi ambazo mara nyingi zimekuwa zikijirudia mara kwa mara” Na mwisho aliwashukuru wadau wote waliofika katika mafunzo hayo na aliwatakia safari njema kwa wote waliosafairi kutoka katika maeneo mbalimbali.