BODI YA WAKURUGENZI COASCO YASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA SHIRIKA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi COASCO CPA. Juma J. Kimori amewataka Menejimenti ya Shirika kuhakikisha kuwa wanaendeleza kazi ya ukaguzi wa kina kwa vyama vya Ushirika na kuhakikisha kuwa vyama vyote vinakaguliwa ipasavyo ili kudhibiti ubora na uwazi. Na pi Menejimenti iweke mikakati ya kuongeza uzalishaji na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.
CPA. Kimori ameyasema hayo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika tarehe 21 Agosti 2025 katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF uliopo Jijini Dodoma
“Hakikisheni mnafanya Ukaguzi wa kina na wenye Tija kwa Vyama vya Ushirika kwa ubora na uwazi na pia boresheni utumiaji wa Teknolojia kwa Kujenga mifumo ya kisasa ya teknolojia kwa huduma bora zaidi na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima”
Aliongeza kuwa kuwe na Ufuatiliaji wa Sera za Umma na Kuhakikisha vyama Ushirika nchini vinatekeleza hilo, na kutoa ushauri na elimu mbalimbali ni wajibu wetu ili Kujenga viongozi wazuri watakaoendelea kuongoza vyama kwa muda mrefu,
Na mwisho amewashukuru Menejimenti na Watumishi wa Shirika kwa kushiriki kujenga sekta yenye uwazi na uwajibikaji na kwa Kazi nzuri inaendelea ya kuboresha huduma na kuongeza uwezo wa vyama vya ushirika nchini