CPA. Golden Kajaba Ahitimisha Mafunzo kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika Jijini Dodoma
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limehitimisha kwa mafanikio mafunzo makubwa ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika Jijini Dodoma. Mafunzo haya yamelenga kuimarisha uongozi na utendaji bora katika sekta ya ushirika nchini na kujifunza kuhusu Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2025, ambayo yatasaidia kuelewa athari za sheria mpya kwenye biashara katika undeshaji wa shughuli za Vyama vya Ushirika, na ili waweze kuchua hatua zinazostahili kwa wakati na kusaidia kuboresha ufanisi, kuongeza imani ya wanachama na kuhakikisha ushirika unakuwa nguzo thabiti ya maendeleo ya taifa.