Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
DAHRAM – WIZARA YA KILIMO AFANYA ZIARA COASCO
DAHRAM – WIZARA YA KILIMO AFANYA ZIARA COASCO Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. James Kibamba, amefanya ziara katika ofisi za Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kwa lengo la kujitanbulisha pamoja na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika hilo. Katika ziara hiyo, Bw. Kibamba alipokelewa na uongozi wa COASCO ambapo alipata maelezo kuhusu majukumu, mipango, na mafanikio ya Shirika hilo katika kuhakikisha uwajibikaji, uwazi, na usimamizi bora wa vyama vya ushirika nchini. Aidha, alitumia fursa hiyo kupongeza kazi kubwa inayofanywa na COASCO katika kusimamia maendeleo ya sekta ya ushirika na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Kilimo na COASCO katika kutekeleza majukumu ya Serikali ya kuboresha huduma kwa wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika. Kwa upande wake, uongozi wa COASCO ulitoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo kupitia Bw. Kibamba kwa kutenga muda wa kufika COASCO, na kuahidi kuendeleza ubunifu na ufanisi katika utoaji wa huduma za ukaguzi na usimamizi wa vyama vya Ushirika kote nchini.