Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
DKT. STEPHEN NINDI, AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA SHIRIKA LA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA (COASCO)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi, amefanya ziara ya kikazi katika Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) Jijini Dodoma na amesisitiza kuendelea kuunda na kuimarisha mifumo mbalimbali ya kidigitali ya Ukaguzi ili kuweza kufanya kaguzi bora katika Vyama vya Ushirika na kuongeza tija kwenye Vyama na wanaushirika kwa ujumla, Ameelekeza hayo tarehe 21 Februari 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye Makao Makuu ya Shirika kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza maoni na changamoto mbalimbali zinazolikabili, Dkt. Nindi amesisitiza kuwa kama Shirika inabidi tuwaze kimkakati na kuweza kujua ndoto zetu na tutazifikiaje na tuongeze ufanisi katika kazi zetu ili tuweze kufikia malengo, Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Coasco CPA. Jeremiah J. Mugeta amewaasa Watumishi wa Coasco kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni kwani lengo kuu ni kuhudumia wananchi kupitia sekta hii ya Ushirika kwa kufanya Ukaguzi na Usimamizi kwa Vyama vya Ushirika Pamoja na Ushauri katika masuala yahusuyo kodi za aina mbalimbali’ Na amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kuja kutembelea Ofisi za Shirika Pamoja na kuongea na Watumishi kutoka Makao Makuu na Ofisi yetu ya Kanda ya Dodoma.