Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama Vya Ushirika (COASCO) limekabidhiwa magari matano ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama Vya Ushirika (COASCO) limekabidhiwa magari matano ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. Magari hayo ni kati ya magari 38 kwenye Taasisi mbali mbali zilizo chini ya Wizara hiyo Pamoja na mitambo ya uchimbaji visima, itakayotumika katika shughuli za Wizara na Taasisi zake za umwagiliaji. Akikabidhi magari hayo kwa COASCO alisema, wameanza kuisaidia COASCO ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. “Angalau tumeanza kuisaidia COASCO ili iweze kutimiza wajibu wake, tunaamini performance ya COASCO kwani sasa hivi wana resources za kibajeti wameanza kupata, vitendea kazi wameanza kupata ili waweze kutimiza wajibu na kuonesha value for money na anaamini vision ya COASCO itabadilika” alisema Pia Waziri huyo alisema Wizara yake inatarajia kuanzisha mpango wa ruzuku ya uchimbaji visima kwa ajili ya wakulima wa kipato cha chini, ambapo visima vitachimbwa bila malipo. Alisema kuwa kupitia mpango huo, wakulima watanufaika kwa kuanza kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua zisizo na uhakika, hivyo kuongeza tija kwenye kilimo. Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Mweli alisema kuwa ujio wa magari hayo COASCO kutaongeza ufanisi, “Kimsingi COASCO walikuwa na hali mbaya na nakumbuka Waziri ulielekeza tuongeze bajeti na tununue vitendea kazi kwa ajili ya Shirika hilo na tumetekeleza na leo utawakabidhi magari matano”