Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
COASCO IMEFANYA MAFUNZO YANAYOHUSU MASUALA YA UKIMWI, LISHE NA RUSHWA
20 Dec, 2024
COASCO IMEFANYA MAFUNZO YANAYOHUSU MASUALA YA UKIMWI, LISHE NA RUSHWA

SHIRIKA LA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA (COASCO) LIMEFANYA MAFUNZO YANAYOHUSU MASUALA YA UKIMWI, LISHE NA RUSHWA KWA WATUMISHI WAKE

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi CPA. Golden Kajaba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Coasco amesema “Tujitahidi kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya zetu, na mazoezi hayo sio lazima yawe ya kukimbia au kunyanyua vyuma bali hata kwa kutembea angalau nusu saa kwa siku inatosha, afya ndio mtaji mkuu katika kuimarisha Utumishi wetu”,

Naye mkufunzi na mwezeshaji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dr. Muhsin Chikota ameeleza kuwa, kwa sasa tatizo la Magonjwa yasiyoambukiza linazidi kushika hatamu kwa watu wengi kwa kutokufanya mazoezi na ulaji wa kupitiliza, mfano wa magonjwa hayo ni Kisukari, Shinikizo la Juu la Damu, Saratani, Mfumo wa upumuaji, afya ya akili, na ya kurithi kama vile selimundu. Magonjwa haya yanaongezeka kwa kasi na kuwaathiri hata watu wenye umri mdogo wakiwemo watoto. 2023, watu mil 42 (74% ya vifo vyote) walifariki duniani kote kutokana na magonjwa haya na 86% ya vifo vyote vinavyohusu watu wenye miaka 30-70 husababishwa na magonjwa haya,

Pia mtaalamu mwandamizi wa lishe kutoka Hospitali ya Jiji la Dodoma Bi, Semeni K. Juma amesisitiza kuwa kuzingatia lishe ni jambo bora sana kwani linaweza kukupa picha ya mwelekeo wa afya yako leo na hata baadae,

Mada kuhusu rushwa yalimewasilishwa na Mtaalam kutoka katika ofisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Ndg Malecha na amesisitiza kuikataa rushwa kuanzia ngazi ya jamii,

Mafunzo hayo yalifungwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Coasco CPA. Prisilla Mushi, ambaye kwa ujumla alisisitiza na kuwaasa watumishi kuzingatia mafunzo hayo na pia amewataka Watumishi wa Shirika kuongeza weledi na ufanisi katika kufanya kazi zao za kila siku.