SHIRIKA LA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA (COASCO) LIMEFANYA MAFUNZO YA WAKAGUZI

SHIRIKA LA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA (COASCO) LIMEFANYA MAFUNZO YA WAKAGUZI KUANZIA TAREHE 29 - 31 JANUARI 2025 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA NSSF KATIKA MANISPAA YA MOROGORO
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika CPA Jeremiah J. Mugeta amesema “Mafunzo haya yanalenga kuboresha ukaguzi tunaoufanya na kuongeza thamani ya kazi za ukaguzi kwa wateja wetu. Hali kadhalika mafunzo haya yataboresha utunzaji kumbukumbu wa kazi za ukaguzi tunazofanya na kurahisisha ufuatiliaji wa usahihi wa ripoti zinazotolewa kwa wateja. Natambua kabla ya mafunzo yanayokwenda kufanyika hapa, tumefanya mafunzo ya awali katika mikoa yenu ambayo lengo lake lilikuwa kujengo uwezo katika masuala ya msingi yanayohusu ukaguzi na uandishi wa ripoti za ukaguzi.
Pia mafunzo hayo yamehudhuriwa na Menejimenti ya Shirika Pamoja na Wakaguzi wa Shirika kutoka katika mikoa ya Tanzania bara
Mmoja kati ya Wakaguzi hao CPA Elice Mmari amesema kuwa “Nipo hapa Morogoro kuhudhuria mafunzo ya mfumo wa Ukaguzi wa taarifa za fedha unaojulikana kwa jina la COADMIS ambao umerahisiha sana kazi za ukaguzi ukilinganisha na mfumo tuliokuwa tunautumia hapo awali”
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo CPA Edson Paschal Mutalemwa amesema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuondoa gharama za shajala Pamoja na kurahisisha mawasiliano baina ya vyama vya Ushirika na Wakaguzi na pia utaokoa muda wa kufanya kaguzi katika vyama husika
CPA Mugeta amewataka wakaguzi wote kuzingatia mafunzo haya ili kuleta tija katika masuala yote ya Ukaguzi na uandishi wa vitabu kwa Vyama