Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na mikopo (ICUD) 2024
22 Oct, 2024
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na mikopo (ICUD) 2024

USHIRIKA UPO, NGUVU YAKE NI KUBWA NA UPO SEHEMU SALAMA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (Mb) amefungua maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na mikopo (ICUD) 2024 katika viwanja vya Milongo Jijini Mwanza yaliyoanza tarehe 20 – 24 Oktoba, 2024

Mhe. Silinde amesema kuwa na wingi wa watu na idadi kubwa ya Washiriki katika Maadhimisho haya ya ICUD 2024 hapa Jijini Mwanza kunaonesha kuwa Ushirika upo hai na nguvu yake ni kubwa na upo sehemu salama

“Kuendelea kuadhimisha siku hii muhimu hapa nchini kunasaidia kuwakumbuka waliosimamia Ushirika huu na kuuonesha Ulimwengu kuwa Ushirika unathamini jasho na nguvu za wale walioitumikia kwa weledi na Uadilifu”

Pia amewaomba viongozi wote kusimamia Ushirika kwa kufuata maadili ya uongozi, sheria na taratibu ili kuendelea kuimarisha vyama vyetu na kuendelea kujenga na kuimarisha uchumi wetu