COASCO & ACFE WAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA UCHUNGUZI KWA WAKAGUZI
COASCO & ACFE WAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA UCHUNGUZI KWA WAKAGUZI
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu Tanzania (ACFE), wameendesha mafunzo maalum kwa wakaguzi wa Shirika wanaohusika na masuala ya uchunguzi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Uzunguni Park jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, CPA Jeremiah Mugeta, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa mbinu bora za kisasa za kufanya uchunguzi na uandishi wa ripoti za uchunguzi zenye viwango vya juu vya kitaalamu.
Kwa upande wake, Rais wa ACFE Tanzania, CFE Ali Mabrouk Juma, amesema mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuongeza uelewa wa kitaalamu kuhusu uchunguzi wa udanganyifu.
Mafunzo hayo yalianza tarehe 20 na kufikia tamati tarehe 24, 2026.
Naomba upitie na hizo
