KAMATI YA BODI YA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VIHATARISHI COASCO YAJADILI TAARIFA MBALIMBALI KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA
KAMATI YA BODI YA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VIHATARISHI YAJADILI TAARIFA MBALIMBALI KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha kikao cha Kamati ya Bodi ya Ukaguzi na Usimamizi wa Vihatarishi ili kujadili ripoti ya Mkaguzi wa ndani, taarifa ya Usimamizi wa vihatarishi na Taarifa ya kifedha ya Shirika kwa lengo la kuzidi kuimarisha utendaji wa Shirika.
Kikao hicho kimefanyika leo, Agosti 27, 2026, katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CPA Aziz Dachi. Kikao hicho pia kiliwakutanisha wajumbe wa Kamati hiyo na Menejimenti ya COASCO.
Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa COASCO kinachotarajiwa kufanyika Septemba 2, 2026, ambapo taarifa na mapendekezo yaliyopitiwa yatawasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi.
