Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI
03 Mar, 2026
BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI

BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA COASCO YAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI 

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wamepatiwa mafunzo ya kutambua, kutathmini, kuangalia na kudhibiti vihatarishi (Risk Management) ili kuongeza ufanisi wa ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Ushirika.

Akizungumza wakati wa mafunzo haya yaliofanyika leo Februari 24, 2026 katika Ofisi ya Makao Makuu ya COASCO, Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanakabiliana na vihatarishi.

“Ili Shirika liende mbali zaidi ni lazima lijue vihatarishi vilivyo mbele yake na namna gani itakabiliana navyo hivyo mafunzo haya ya `Risk Management ` yatatuongezea uelewa Zaidi na kupelekea Shiriki lizidi kutoa huduma bora za ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Ushirika” amesema CPA. Mugeta

Naye, Mkufunzi wa mafunzo hayo, CPA Cosmas Mbogela kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, alibainisha kuwa kuanzisha mfumo thabiti wa kutambua vihatarishi na njia sahihi ya kuvidhibiti ni hatua muhimu katika ukuaji wa Shirika.