Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
COASCO: HATI SAFI ZA VYAMA VYA USHIRIKA ZAPANDA HADI ASILIMIA 20
09 Aug, 2026
COASCO: HATI SAFI ZA VYAMA VYA USHIRIKA ZAPANDA HADI ASILIMIA 20

COASCO: HATI SAFI ZA VYAMA VYA USHIRIKA ZAPANDA HADI ASILIMIA 20

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika Tanzania (COASCO) limesema idadi ya vyama vya ushirika vinavyopata hati safi za ukaguzi imeongezeka kutoka asilimia 16 mwaka 2024/2025 hadi asilimia 20 mwaka 2025/2026.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, jijini Dodoma wakati akielezea majukumu ya shirika hilo na kueleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, vyama vilivyopata hati safi vimeongezeka kwa asilimia nne, kutoka asilimia 16 hadi asilimia 20.

CPA Mugeta amesema ongezeko hilo linaonesha kuimarika kwa usimamizi wa fedha na uwajibikaji katika vyama vya ushirika, huku akisisitiza kuwa mafunzo yanayotolewa na COASCO kwa viongozi na watendaji yamechangia kuboresha matokeo ya ukaguzi.

Amesema COASCO itaendelea kutoa huduma za ukaguzi, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa vyama vya ushirika ili kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za wanachama.