COASCO imefanya mkutano cha baraza kuu la Wafanyakazi Jijini Dodoma
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika tarehe 20 Disemba, 2024 limefanya mkutano cha Baraza kuu la Wafanyakazi katika ukumbi wa PSSSF hapa Jijini Dodoma
Katika Mkutano huo ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu CPA Jeremiah J. Mugeta na kuhudhuriwa na wajumbe wa baraza hilo amesema kuwa “anawashukuru Wajumbe wote kwa kuwa wasikivu, wavumilivu na kuishauri vema Menejimenti katika kufanikisha na kutekeleza mkataba wa hali bora kwa Watumishi ikiwemo na maendeleo katika utendaji kazi wa Shirika”
Naye mwakilishi wa chama cha wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) amesema kuwa pamoja na majukumu mengine lakini badowanaendelea kutoa Elimu kwa wanachama,Viongozi na Wafanyakazi juu Sheria na mbinu za majadiliano, kujadili na kufunga mikataba ya hali bora (CBA) baina ya Chama na Waajiri na pia kusimamia utekelezaji wa Mikataba, Maazimio na Matakwa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yaliyoridhiwa na Nchi yetu