KAMATI YA BODI YA MIPANGO NA UCHUMI YAKUTANA KUIMARISHA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USIMAMIZI KWA MANUFAA YA VYAMA VYA USHIRIKA
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha Kikao cha 85 cha Kamati ya Bodi ya Mipango na Uchumi kwa lengo la kujadili hali ya utendaji wa Shirika na mwelekeo wa Mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo (2026-
2031), ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza tija, uwajibikaji na ustawi wa Vyama vya Ushirika nchini.
Katika kikao hicho, wajumbe walijadili kuhusu uwekezaji wa miradi ya ubia kwa lengo la kuongeza mapato ya Shirika hilo, pamoja na kupitia taarifa za utendaji kutoka Kurugenzi na Vitengo mbalimbali ili kuimarisha huduma za ukaguzi na usimamizi kwa manufaa ya Vyama vya Ushirika.
Kikao hicho kimefanyika leo, tarehe 26 Februari, 2026 katika Ukumbi wa Shirika Ofisi ya Dodoma Makao Makuu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo kinachotarajiwa kufanyika tarehe 27 Februari, 2026.
