Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAKUTANA KUJADILI MASUALA YA UKAGUZI, USIMAMIZI WA VIHATARISHI, AJIRA, MAENDELEO YA UTUMISHI NA UTAWALA
03 Mar, 2026
KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAKUTANA KUJADILI MASUALA YA UKAGUZI, USIMAMIZI WA VIHATARISHI, AJIRA, MAENDELEO YA UTUMISHI NA UTAWALA

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha vikao vya Kamati ya Bodi ya Ajira na Maendeleo ya Utumishi na Utawala pamoja na Kamati ya Bodi ya Ukaguzi na Usimamizi wa Vihatarishi kwa lengo la kupitia na kujadili masuala mbalimbali ya sheria, miongozo, rasilimali watu, ajira na maendeleo ya watumishi, sambamba na kuchambua mapendekezo yaliyowasilishwa na wakaguzi ndani na nje ya Shirika.

Vikao hivyo vimefanyika leo, tarehe 25 Februari, 2026 katika Ukumbi wa Shirika Ofisi ya Dodoma Makao Makuu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika kitakachofanyika tarehe 27 Februari, 2026