Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
COASCO YAUNGANA NA FAMILIA YA MAREHEMU RASHID MRISHO KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA
30 Apr, 2026
COASCO YAUNGANA NA FAMILIA YA MAREHEMU RASHID MRISHO KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA

COASCO YAUNGANA NA FAMILIA YA MAREHEMU RASHID MRISHO KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA

Watumishi wa COASCO wameungana na familia ya marehemu Rashid Mrisho, aliyekuwa Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, katika mazishi yaliyofanyika leo tarehe 29 Aprili 2026, kijijini kwao Manoleo, kilichopo Manispaa ya Tabora 

Uongozi wa COASCO uliwakilishwa na CPA Denis Barongo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, CPA Jeremiah Mugeta, kwa ajili ya kutoa pole na faraja kwa ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo.

Marehemu atakumbukwa kwa uchapakazi, nidhamu ya hali ya juu na kujituma katika utekelezaji wa majukumu yake.

COASCO inaendelea kuiombea familia faraja, subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.