COASCO YAZIDI KUIMARISHA UTENDAJI KUPITIA VIKAO VYA WATUMISHI VYA KILA MWEZI
COASCO YAZIDI KUIMARISHA UTENDAJI KUPITIA VIKAO VYA WATUMISHI VYA KILA MWEZI
Watumishi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wamefanya kikao cha kila mwezi kwa lengo la kusikiliza maoni, mapendekezo na changamoto mbalimbali ili kuimarisha utendaji wa Shirika.
Kikao hicho kimefanyika Machi 25, 2026 katika Ofisi ya Makao Makuu ya COASCO jijini Dodoma, na kuongozwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, CPA Prisilla Mushi, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, CPA Jeremiah Mugeta.
Katika kikao hicho, CPA Mushi amesisitiza umuhimu wa watumishi kujaza PEPMIS kutokana na uhalisia wa majukumu wanayofanya, kufanya kazi kwa umoja, kuimarisha ushirikiano, kuzingatia nidhamu ya kazi pamoja na kuepuka vitendo vya rushwa.
Mkugenzi wa Utafiti na Ushauri CPA Golden Kajaba na Meneja Rasilimali watu na Utawala wa Shirika hilo, Vicent Bukombe wamesisitiza kufanyika kwa vikao hivyo vya watumishi kwa kila mwezi ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Shirika na ustawi wa watumishi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuboresha huduma za Shirika.
