COASCO & TCDC ZAKUTANA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI
28 May, 2026
COASCO & TCDC ZAKUTANA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI
Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wamekutana kupokea taarifa ya kamati maalum kuhusu namna bora ya kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya ushirika nchini.
Kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel G. Chongolo, ya kuendelea kuimarisha sekta ya ushirika nchini.
Kikao hicho kimefanyika leo, Mei 22, 2026 katika ofisi ya Mrajis wa TCDC, kikiongozwa na Mtendaji Mkuu na Mrajis wa TCDC, Dkt. Benson O. Ndiege.
