Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
COASCO YAWANOA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA KODI, EXCEL NA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA
27 Apr, 2026
COASCO YAWANOA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA KODI, EXCEL NA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA

COASCO YAWANOA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA KODI, EXCEL NA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA


Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limewajengea uwezo watendaji wa vyama vya ushirika kwa kutoa mafunzo ya kodi, matumizi ya Excel, uandaaji wa taarifa za fedha pamoja na taarifa za uendelevu, kwa lengo la kuboresha utendaji wa vyama hivyo.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo, Aprili 22, 2026 katika Ukumbi wa Morena jijini Morogoro na Mkurugenzi wa Utafiti na Ushauri wa Shirika hilo, CPA Golden Kajaba, ambaye amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu.

“Mafunzo haya yameandaliwa kwa kuzingatia mazingira ya sasa ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa kuzingatia mabadiliko ya viwango vya kimataifa vya uhasibu,” amesema CPA Kajaba.

Aidha, ameongeza kuwa mafunzo hayo ni uwekezaji muhimu katika kuimarisha utawala bora, uwazi, ufanisi na uendelevu wa sekta ya ushirika nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Ushauri na Mafunzo wa Shirika hilo, CPA Denis Barongo, amesema zaidi ya washiriki 270 kutoka vyama mbalimbali wameshiriki mafunzo hayo ya siku tatu yanayoendelea kuanzia Aprili 22 hadi 24, 2026.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Hellen Lungo ambaye ni Mhasibu wa UWAWAKUDA SACCOS Limited, amesema mafunzo hayo yatamsaidia kuongeza ujuzi na ufanisi katika uandaaji wa taarifa za fedha na kuboresha utendaji wa chama ili kuendelea kupata hati ya ukaguzi inayostahili.