Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WIZARA YA KILIMO, COASCO ZAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA
13 Aug, 2026

Kurugenzi ya Masoko na Usalama wa Chakula ya Wizara ya Kilimo imefanya kikao kazi na Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kwa lengo la kupitia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Daniel G. Chongolo Waziri wa Kilimo na kujadili mipango, changamoto zilizopo, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa huduma za Shirika.
 
Kikao hicho kimefanyika Agosti 8, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Makao makuu ya Shirika jijini Dodoma, kikiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Usalama,  Happy Kitingati, akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Kilimo.
 
Kikao hicho ni sehemu ya ushirikiano kati ya Wizara ya Kilimo kupitia Kurugenzi ya Masoko na Usalama wa Chakula na COASCO katika kuimarisha ukaguzi, usimamizi, uwajibikaji na ufanisi wa sekta ya ushirika nchini.