Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO MPYA WA e-BOARD
03 Mar, 2026
BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO MPYA WA e-BOARD

BODI YA WAKURUGENZI YA COASCO YAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO MPYA WA e-BOARD

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imepatiwa mafunzo maalum ya matumizi ya mfumo mpya wa e-Board, kwa lengo la kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na usimamizi wa vikao vya Bodi kwa njia ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo, Februari 24, 2026, katika Ofisi ya Makao Makuu ya COASCO jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo CPA. Jeremiah Mugeta amesema kuwa mfumo wa e-Board utarahisisha uendeshaji wa vikao kwa njia ya kidijitali pia utamuwezesha mjumbe wa Bodi kushiriki kikao hata akiwa mbali na eneo la kikao.

 “ Mafunzo haya yamelenga kuhakikisha wajumbe wa bodi wanajengewa uwezo wa matumizi ya mfumo huu utakaowawezesha kufanya vikao kwa njia ya mtandao (online) bila kuathiri ubora wa maamuzi ya bodi, pamoja na kuandaa, kusambaza na kuhifadhi nyaraka za vikao kwa njia salama na ya kisasa” amesema CPA. Mugeta 

Kwa upande wake, Mkufunzi kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Mwanamvua Rasi, amesema mafunzo hayo ni hatua muhimu kwa shirika kwani yatapelekea kupungua kwa gharama za uendeshaji wa vikao hivo kwa kuondoa matumizi ya karatasi na uchapishaji.