MWALIKO WA MAFUNZO YA KITAALAM KWA BODI NA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA KUHUSU MASUALA YA UONGOZI, KODI, UHASIBU NA TEHAMA
📢 TANGAZO LA MAFUNZO KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo maalum yatakayofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Juni, 2026 katika Ukumbi wa Destiny – Kibaha.
Mafunzo haya yamelenga kuongeza ufanisi na uwezo wa kiutendaji katika maeneo muhimu ya:
✅ Uongozi na Utawala Bora
✅ Kodi na Usimamizi wa Mapato
✅ Uhasibu na Usimamizi wa Fedha
✅ Matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Vyama vya Ushirika
Gharama zamafunzo kwa kila mshiriki ni Tshs 350,000 ambayo inajumuisha mafunzo ya siku tatu, ukumbi, chai na chakula cha mchana. Malipo hayo yatalipwa kupitia nambari ya malipo ya Serikali itakayotolewa baada ya kuthibitisha ushiriki wako kwa kuwasiliana na RCA au mratibu wa mfunzo (CPA Anna Thomas) kupitia nambari ya simu 0658 732 050 au barua pepe anna.shao@coasco.qo.tz
Washiriki watapata mafunzo ya nadharia na vitendo yatakayowawezesha kuongeza tija, uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Usikose fursa hii muhimu ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mtandao wa kitaaluma na viongozi wengine wa ushirika. Karibuni sana tujifunze pamoja kwa maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.
COASCO — Ukaguzi wa Uhakika, Ushirika Imara!
