KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA KILIMO SABASABA
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA COASCO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA KILIMO SABASABA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Jeremiah Mugeta, ametembelea banda la Wizara ya Kilimo na taasisi zake zinazoshiriki katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo imefanyika Julai 8, 2026, ambapo CPA Mugeta alitembelea mabanda ya TCDC, ASA, TOSCI, COPRA, TARI, TPHPA, TFRA, NFRA, AGITF, Bodi ya Sukari, Bodi ya Mkonge na Bodi ya Pamba, na kupata fursa ya kujionea huduma, teknolojia na ubunifu mbalimbali unaotekelezwa na taasisi hizo katika kuendeleza sekta ya kilimo na ushirika.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano kati ya COASCO na taasisi za Wizara ya Kilimo, kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yanayolenga kukuza sekta ya ushirika na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Taifa
Aidha, CPA Mugeta amevishauri Vyama vya Ushirika vya Mazao kuyaongezea thamani mazao ya kilimo ili kupata bei nzuri katika masoko ya ndani ya nchi na ya kimataifa.
