Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
KAMATI YA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VIHATARISHI COASCO YAPITIA TAARIFA MBALIMBALI KWA LENGO LA KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA
03 Nov, 2026

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha kikao cha Kamati ya Ukaguzi na Usimamizi wa vihatarishi kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya mkaguzi wa ndani, usimamizi wa vihatarishi pamoja na sera na miongozo ya ulinzi wa taarifa binafsi za Shirika, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utendaji na mifumo ya usimamizi wa Shirika.

Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CPA Aziz Dachi, tarehe 2 novemba 2026 na kuwakutanisha wajumbe wa Kamati pamoja na Menejimenti ya COASCO. Kimefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma.

Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha 88 cha Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika, kinachotarajiwa kufanyika jijini Dodoma tarehe 6 Novemba 2026.