BODI YA COASCO YAMTEUA CPA ALPHONCE MURO KUWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA
02 Sep, 2026
BODI YA COASCO YAMTEUA CPA ALPHONCE MURO KUWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imemteua na kumtambulisha rasmi CPA Alphonce Muro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo na kutambulishwa rasmi katika Bodi.
Utambulisho huo umefanyika leo, Septemba 2, 2026, wakati wa Kikao cha 87 cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika katika hoteli ya Best Western jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO, CPA Juma A. Kimori, amempongeza na kumkaribisha rasmi kwa wajumbe wa Bodi, huku akimtakia mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.
Kabla ya uteuzi huo CPA Muro alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani katika Wizara ya Ardhi.
