Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAJADILI MASUALA MBALIMBALI ILI KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA
06 Nov, 2026
KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAJADILI MASUALA MBALIMBALI ILI KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA

KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAJADILI MASUALA MBALIMBALI ILI KUIMARISHA UTENDAJI WA SHIRIKA

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha vikao vya Kamati ya Mipango na Uchumi pamoja na Kamati ya Ajira, Maendeleo ya Utumishi na Utawala kwa lengo la la kupitia masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Shirika.

Kikao cha Kamati ya Mipango na Uchumi, kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Benson Ndiege, kilifanyika Novemba 3 2026, huku Kamati ya Ajira, Maendeleo ya Utumishi na Utawala kimeomgozwa na Mwenyekiti Prof. Alfred Sife, ikifanya kikao chake leo, Novemba 4 2026 kwa kushirikisha wajumbe na Menejimenti ya Shirika.

Vikao hivyo ni sehemu ya maandalizi ya Kikao cha 88 cha Bodi ya Wakurugenzi ya COASCO kinachotarajiwa kufanyika Novemba 6 2026, jijini Dodoma.