Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
BODI YA WAKURUGENZI COASCO YAHIMIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YAKE ILI KULETA TIJA KATIKA SHIRIKA
09 Nov, 2026
BODI YA WAKURUGENZI COASCO YAHIMIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YAKE ILI KULETA TIJA KATIKA SHIRIKA

BODI YA WAKURUGENZI COASCO YAHIMIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YAKE ILI KULETA TIJA KATIKA SHIRIKA

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imehimiza Menejimenti ya Shirika kuhakikisha maazimio ya Bodi yanatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika.

Msisitizo huo umetolewa Novemba 6, 2026, na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, CPA Juma Kimori, wakati akiongoza Kikao cha 88 cha Bodi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Best Western jijini Dodoma.

CPA Kimori amesisitiza kuwa utekelezaji wa maazimio ya Bodi ni muhimu katika kufanikisha malengo ya Shirika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Alphonce Muro, ameishukuru Bodi kwa maelekezo na mwongozo wake, akieleza kuwa Menejimenti itaendelea kuyazingatia katika usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya Shirika.