Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
WATUMISHI WA COASCO WANUFAIKA NA MAFUNZO YA AFYA, MAZINGIRA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
19 Jul, 2026
WATUMISHI WA COASCO WANUFAIKA NA MAFUNZO YA AFYA, MAZINGIRA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

WATUMISHI WA COASCO WANUFAIKA NA MAFUNZO YA AFYA, MAZINGIRA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha mafunzo kwa watumishi wake kuhusu mapambano dhidi ya rushwa mahali pa kazi, matumizi ya nishati safi, uhifadhi wa mazingira, UKIMWI na afya ya akili kwa lengo la kuongeza uelewa na kuboresha ustawi wa watumishi katika mazingira ya kazi.

Mafunzo hayo yamewashirikisha watumishi wa Makao Makuu na wa Ofisi ya Kanda ya Dodoma, ambapo yamefunguliwa leo Juni 26, 2026 katika Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, amewahimiza watumishi kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kufahamu hali zao za kiafya na kuchukua hatua stahiki kwa wakati.

Aidha, CPA Mugeta amewaasa watumishi wa Shirika kujiepusha na vitendo vya rushwa mahali pa kazi, akieleza kuwa rushwa ni kikwazo kwa haki, uwajibikaji na maendeleo ya taasisi.

Katika mafunzo hayo, watumishi wa Shirika pia walipata fursa ya kupima afya zao, ikiwemo kisukari, shinikizo la damu , malaria na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), hatua iliyolenga kuhamasisha utamaduni wa uchunguzi wa afya na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kwa upande wake, Issa Msuya, kwa niaba ya watumishi wenzake, ameushukuru uongozi wa COASCO kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema yamewaongezea uelewa na maarifa yatakayowasaidia kuboresha utendaji kazi na kutunza afya zao.