Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

COASO Logo
MENEJIMENTI, WAKAGUZI WA MIKOA NA MAKAO MAKUU COASCO WAJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UTENDAJI WA SHIRIKA
19 Jul, 2026
MENEJIMENTI, WAKAGUZI WA MIKOA NA MAKAO MAKUU COASCO WAJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UTENDAJI WA SHIRIKA

MENEJIMENTI, WAKAGUZI WA MIKOA NA MAKAO MAKUU COASCO WAJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UTENDAJI WA SHIRIKA

Menejimenti, Wakaguzi wa Mikoa na Wakaguzi wa Ofisi ya Makao Makuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wamekutana kufanya tathmini ya utendaji wa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuweka mikakati ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa lengo la kuboresha utendaji wa Shirika.

Akifungua kikao hicho Julai 10, 2026, katika Hoteli ya Palace iliyopo jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, amesisitiza kutumia siku mbili za kikao hicho kujadili kwa uwazi mafanikio, changamoto na kuweka mikakati itakayoboresha utekelezaji wa majukumu ya Shirika.

“Kikao hiki kitajadili taarifa za utendaji wa mwaka 2025/2026, mipango ya mwaka 2026/2027, utekelezaji wa tozo ya shilingi mbili kwa kilo ya mazao yanayouzwa kupitia Vyama vya Ushirika pamoja na maboresho ya mifumo ya COADMIS na CADIS ili kuongeza ufanisi wa Shirika,” amesema CPA Mugeta.

CPA Mugeta amewapongeza watumishi kwa kufanikisha utekelezaji wa zaidi ya asilimia 90 ya malengo ya mwaka wa fedha 2025/2026 na kusisitiza Menejimenti itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha malengo ya mwaka huu wa fedha yanafikiwa kikamilifu