VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAJENGEWA UWEZO KATIKA KODI, FEDHA NA UENDELEVU
26 Sep, 2026
Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika wanaendelea kujifunza kuhusu kodi, sheria za kodi, Muhtasari wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2026, utayarishaji wa taarifa za fedha za mwisho wa mwaka kwa kuzingatia IAS 7, pamoja na ESG na utoaji wa taarifa za uendelevu kwa kuzingatia IFRS S1 na IFRS S2.
Mafunzo hayo yanaendelea leo, Septemba 24, 2026, katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma, ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza Septemba 23 na yanatarajiwa kuhitimishwa kesho, Septemba 25, 2026.
Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha usimamizi na ulinzi wa rasilimali za wanachama na kuboresha uendeshaji wa Vyama vya Ushirika, kupitia kuwajengea uwezo katika maeneo muhimu ya kiutendaji.
