WIZARA YA KAZI,AJIRA,VIJANA NA UWEZESHAJI- ZANZIBAR NA COASCO KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USHAURI WA VYAMA VYA USHIRIKA
WIZARA YA KAZI,AJIRA,VIJANA NA UWEZESHAJI- ZANZIBAR NA COASCO KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USHAURI WA VYAMA VYA USHIRIKA
Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji Zanzibar na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) zimejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma za ukaguzi na ushauri kwa vyama vya ushirika vilivyopo Zanzibar.
Majadiliano hayo yalifanyika Novemba 20, 2026, katika Ofisi za Wizara hiyo Zanzibar,wakati wa ziara iliyofanywa na Viongozi wa COASCO iliyolenga kujitambulisha na kubaini maeneo ambayo COASCO inaweza kupanua huduma zake.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Khalid Masoud Wazir, amesema Wizara ipo tayari kushirikiana na COASCO, akieleza kuwa ushirikiano huo utakuwa fursa muhimu kwa Wizara na vyama vya ushirika Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Alphonce Muro, alisema kuwa pande hizo mbili zinaweza kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) utakaoweka msingi wa ushirikiano katika utoaji wa huduma za ukaguzi, ushauri, utafiti, mifumo ya TEHAMA na mafunzo kwa vyama vya ushirika Zanzibar.
Alieleza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika, hususan katika maandalizi ya taarifa za fedha kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.
Katika ziara hiyo ujumbe wa COASCO ulijumuisha Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Kaimu Meneja wa Biashara na Mwanasheria.
