NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA KILIMO AIPONGEZA COASCO KWA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA KILIMO AIPONGEZA COASCO KWA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. Msoffe, ametembelea banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo alioifanya leo Julai 3, 2026, Prof. Msoffe ameipongeza COASCO kwa mchango wake katika kuimarisha usimamizi, uwajibikaji na utawala bora wa vyama vya ushirika nchini kupitia huduma za ukaguzi, ushauri wa kitaalam na mafunzo mbalimbali kwa wadau wa sekta ya ushirika.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa COASCO kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu huduma zake, ikiwemo ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika na Taasisi nyingine ,ushauri wa kitaalam katika masuala ya fedha, kodi, uhasibu, uwekezaji, utawala bora na usimamizi wa vihatarishi, uandaaji wa sera, miongozo na mipango ya biashara pamoja na uchunguzi maalum
