NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA COASCO
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA COASCO
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi, ameridhishwa na huduma zinazotolewa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) baada ya kutembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Akiwa katika banda hilo Julai 5, 2026, Bw. Mbwasi alipata maelezo kuhusu majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na COASCO ikiwemo ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika na Taasisi nyingine, ushauri wa kitaalamu, mafunzo, uchunguzi maalum pamoja na huduma za usimamizi wa vihatarishi.
Baada ya kupokea maelezo hayo, Bw. Mbwasi amepongeza jitihada za COASCO katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora wa vyama vya ushirika nchini, akibainisha kuwa huduma zinazotolewa na Shirika hilo zina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya ushirika na uchumi wa wananchi.
